MAJUKUMU YA BODI
Jukumu la msingi la Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura ya 290 RE 2000 ni kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwenye Halmashauri kwa ajili ya kutekelezea miradi ili kusaidia kuleta maendeleo.
Aidha, kazi ambazo zinapaswa kutekelezwa na Bodi zimeainishwa chini ya Kifungu cha 60 cha Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa Sura ya 290;
1.Kupokea, kusimamia na kuwekeza (invest) fedha za Bodi.
2.Kuzikopesha Mamlaka za Serikali za Mitaa fedha za Bodi, kwa madhumuni ya kutekelezea miradi na huduma nyingine za maendeleo zinazolenga katika kuziongezea mapato na kuboresha utoaji wa huduma.
3.Kutoa msaada wa kifedha kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa njia ya ruzuku, dhamana (guarantees) kwa mikopo itakayoombwa na kupatikana.
4.Kutoa na kuendesha huduma kwa niaba au kwa faida ya Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Haki Miliki@ Bodi ya Mikoya Mikopo ya Serikali za Mitaa