Wataalam katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wanatakiwa kuandaa maandiko ya bora ili kupatiwa mikopo toka kwenye taasisi za fedha katika kuendeleza miradi mbalimbali kwenye ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa.
Kwa kuwa sasa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Benki ya Maendeleo (TIB) kwa pamoja wataweza kupokea na kufanyia kazi maandiko ya miradi ambayo imeandikwa vizuri, na kwa kufuata vigezo vyote vilivyotolewa, maandiko mazuri yatapewa kipaumbele kwa ajili ya kupata fedha za utekelezaji wa miradi iliyoombewa na itakayoombewa fedha
Umuhimu wa kutumia Bodi hii na kuyaona matokeo chanya yaliotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa baada ya kupatiwa mkopo na Bodi, na vilevile Mamlaka za Serikali za Mitaa kujenga utamaduni wa kulipa madeni ya mikopo kwa wakati.
Haki Miliki@ Bodi ya Mikoya Mikopo ya Serikali za Mitaa