Mamlaka za Serikali za Mitaa zimekuwa zikikosa fedha kwa ajili yakuanzisha miradi mikakati katika maeneo yao kubwa likiwa ni ukosefu wa utaalamwa uandishi bora wa maandiko ya miradi husika.
Mafunzokazi haya yalitolewa na Ndg. Daniel Lyakinana Mkuu wa Idaraya Mikopo wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika ukumbi wa mikutano waHalmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale hivi karibuni na kuhudhuliwa na Mkuu wa Halmashauriya Wilaya ya Nyangw’ale Bi. Husna Chambo
“Nimefurahishwa sana kuona mafunzo haya yanafanyika katika kipindihiki ambapo Halmashauri yetu ina uhitaji mkubwa wa kuwa na miradi itakayoiwezeshaHalmashauri yetu kuwa na vyazo bora vya mapato ya kujiendesha”. alisema Bi.Husna Chambo.
Pia aliwashukuru waandaaji wa mafunzo hayo na kuwaasa watumishiwote kutumia utaalam wao na walioupata katika Mafunzo kazi hayo kuboreshauandishi wa maandiko ya miradi watakayo yaandaa ili kuweza kupata fedhazitakazopelekea kutekeleza miradi katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyangw’ale.
Mafunzokazi hayo yaliwashirikisha Wachumi, Wahandisi, MaafisaUgavi, Maafisa Maendeleo ya Jamii na Watunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya yaNyangw’ale. Tayari Mafunzo kazi kama hayo yameshatolewa na yanaendelea kutolewakatika Mikoa na Halmashauri mbali mbali nchi.
Kwa upande mwingine Mkuu wa Idara ya Utawala na Fedha wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa Ndg. Yeremiah Mahinya baada ya kujibu maswali mbali mbali ya washiriki wa mafunzo haya aliwashauri kubuni na kuandikia miradi mbalimbali pamoja na kusisitiza kwa Halmashauri kuweka mikakati mizuri kwa kulipa madeni ya mikopo ndani ya halmashauri zao ili kuiwezesha bodi ya mikopo kukopesha halmashauri nyingine kwa wakati.
Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ipo kisheria na ilianzishwa kwa lengo la kuzikopesha Mamlaka za Serikali za Mitaa ili ziweze kutekeleza miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa wakati.
Haki Miliki@ Bodi ya Mikoya Mikopo ya Serikali za Mitaa