• Malalamiko
    • Wasiliana Nasi
    • MMM
    • Barua pepe za Watumishi
Local Government Loans Board

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Makatibu Waliowahi Kuongoza Bodi
    • Orodha ya Wajumbe wa Bodi
    • Orodha ya Mawaziri TAMISEMI
  • Huduma
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo
  • Machapisho
    • Taarifa
    • Kanuni
    • Kuomba Mkopo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
  • Miradi
    • Miradi iliyokwisha
    • Mwongozo wa Uombaji wa Mkopo

Kuomba Mkopo

MASHARTI YA KUOMBA MKOPO KATIKA BODI YA MIKOPO YA SERIKALI ZA MITAA

 

Bodi hii ni chombo kilichoanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa ya Mwaka 1982 Sura Na.290. Re. 2002. Lengo kuu la kuanzishwa kwa Bodi ni kutoa fedha kwa njia ya mikopo ili kutekeleza miradi inayolenga kuchochea shughuli za kiuchumi, kuongeza ajira na mapato ya Halmashauri husika.

Kimsingi, Halmashauri inayo fursa ya kukopa katika Bodi ili mradi iwe imetimiza masharti yafuatayo:-

  1. Imekamilisha Mchango wake wa Akiba (Minimum Compulsory Reserve) kwa asilimia 100. 
  2. Halmashauri inatakiwa iandae andiko la mradi (Project Write-up) na kuwasilisha kwenye Bodi.
  3. Mradi husika uwe umepata baraka za Kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri husika.
  4. Mradi uwe mmoja mahsusi, unaotekelezeka na wenye manufaa kiuchumi na kijamii kwa Halmashauri. Aidha Halmashauri inayo fursa ya kukopa tena baada ya kukamilisha mradi uliopata mkopo awali na kurejeshwa.
  5. Halmashauri inatakiwa kuainisha kazi zitakazotekelezwa kwenye mpango kazi utakaoandaliwa kwa kipindi chote cha mradi.
  6. Halmashauri inatakiwa ichangie asilimia 20 ya gharama ya mradi husika. Kwa maana hiyo kiasi cha asilimia 80 ya gharama za mradi ndicho kitakachotolewa na Bodi kwa njia ya mkopo.
  7. Mkopo utarejeshwa katika kipindi cha muda maalum kulingana na ukubwa wa mradi kwa riba ya asilimia kumi na tatu (13%) kwa mwaka kwa sasa.
  8. Marejesho ya mkopo yatatokana na vyanzo vya mapato ya Halmashauri kwa ujumla pamoja na mapato ya mradi husika utakapoanza kufanya kazi.
  9. Marejesho ambayo muda wake utakuwa umepita, riba (penalty) ya asilimia moja (1%) itatozwa.
  10. Halmashauri itatakiwa kuwasilisha taarifa iliyothibitishwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) au taasisi inayotambulika iliyoidhinishwa na Baraza la Usimamizi wa Mazingira kuonyesha jinsi suala la mazingira litakavyosimamiwa ili kuhifadhi mazingira.
  11. Masharti mengine ya mkopo huelezwa kwenye mkataba wa mkopo ambao huandaliwa kwa ajili ya kusainiwa na Halmashauri na Menejimenti ya Bodi kwa mujibu wa makubaliano.

Matangazo

  • RAIS SAMIA AIWEZESHA REA BILIONI 96.8 UTEKELEZAJI MIRADI YA UMEME VIJIJINI DODOMA May 13, 2025
  • TAARIFA KWA UMMA KUHUSU WAHITIMU WA KIDATO CHA NNE,2023 KUFANYA MABADILIKO YA TAHASUSI ZA KIDATO CHA TANO NA KOZI ZA VYUO KWA MWAKA 2024 March 20, 2024
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MWENENDO WA UREJESHAJI MIKOPO KWENYE HALMASHAURI UNARIDHISHA - DKT. FESTO DUGANGE.

    May 08, 2025
  • MAFUNZO YA UANDISHI BORA WA MAANDIKO YA MIRADI ILI KUZIWEZESHA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUPATA PESA ZA MIRADI YA KIMKAKATI

    March 08, 2024
  • MAANDIKO BORA KUZIWEZESHA MAMLAKA ZA SERIKALI ZA MITAA KUPATIWA MIKOPO KWENYE TAASISI ZA FEDHA

    March 25, 2024
  • LAAC: HATUTAKUBALI SERIKALI IPATE HASARA

    March 21, 2024
  • Angalia Zote

Wasiliana Nasi

Local Government Loans Board

Sanduku la Barua: P.O Box 2710

Simu: +255 26 2321730

Barua Pepe: barua@lglb.go.tz

Fax:

Viungo vya Haraka

  • Watumishi Portal
  • President's Office, Regional Adminstration and Local Government
  • MATUKIO

Zinazohusiana

  • Chuo cha Serikali za Mitaa
  • OR-TAMISEMI
  • UTUMISHI
  • TAMISEMI BLOG
  • Benki ya Maendeleo (TIB)

Video Mpya

More Videos
    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Sitemap
    • Huduma

Haki Miliki@ Bodi ya Mikoya Mikopo ya Serikali za Mitaa